Wasanii mbalimbali wa muziki nchini Tanzania wamemuenzi aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli kwa nyimbo mbalimbali zilizojaa hisia, huzuni na majonzi.
Rais Magufuli ambaye alifariki siku ya Jumatano, tarehe 17 Machi, alikuwa karibu sana na wasanii wa Bongo Flava na hata Bongo Movie ambao walishiriki vilivyo kwenye kampeni zake za uchaguzi mkuu.
Tunakuorotheshea nyimbo mbalimbali ambazo zimetolewa kwa ajili ya kumkumbuka na kumuenzi hayati Rais John Pombe Magufuli.