Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amekutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Marekani, Kamala Harris, jijini Washington, D.C. nchini Marekani.
Rais Samia na ujumbe wake ambao wako nchini Marekani kwa ziara ya kikazi, alimtembelea Makamu wa Rais Kamala katika Ikulu ya Marekani au White House na kufanya mazungumzo hayo.
Katika mazungumzo hayo, viongozi hao wawili walisema wamedhamiria kuendeleza ushirikiano baina ya nchi hizi mbili katika nyanja mbalimbali za kiuchumi na kibiashara.
Katika ziara hiyo Rais Samia pia atazindua kipindi cha televisheni cha kuitangaza Tanzania kinachotwa Royal Tour kinachotayarishwa na kutangazwa na Peter Greenberg ambacho kitarushwa katika vituo mbalimbali vya Televisheni nchini Marekani.
Unaweza kuangalia video hii hapo chini yenye dondoo za mkutano wa waandishi wa habari kati ya Rais Samia Sulu Hassan na Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris kwa hisani ya Msema Mkuu wa Serikali.