Msanii wa muziki wa kizazi kipya au kama unavyojulikana na wengi kwa jina la Bongo Flava ambaye pia alikuwa muigizaji wa tamthiliya, Maunda Zorro, amefariki dunia kwa ajali ya gari jijini Dar Es Salaam.

Msanii huyo ambaye ni dada wa msanii Banana Zorro, na pia ni mtoto wa msanii mkongwe wa muziki wa dansi (Zilipendwa) nchini Tanzania, Zahir Ally Zorro.

Maunda Zorro akiwa na Baba yake Msanii mkongwe wa muziki wa dansi Tanzania, Zahir Ally Zorro
Eneo la ajali iliyoondoa uhai wa Maunda Zorro baada ya kugongana na lori la mchanga.

Kulingana na taarifa zilizotufikia, msanii huyo alifariki kutokana na ajali ya gari iliyotokea Kigamboni jijini Dar Es Salaam, Tanzania.

Enzi za uhai wake Maunda Zorro

Ajali hiyo imetokea wakati akitoka kwenye msiba wa rafiki yake anayeitwa Mecky, ambaye alikuwa amefariki siku mbili kabla yake. Kwenye ukurasa wake wa Instagram aliandika ujumbe wa kushtushwa kuhusiana na kifo cha Mecky pasipo yeye kujua kuwa nae angefariki baada ya siku mbili.

Maunda atakumbukwa katika tasnia ya muziki kutokana na uimbaji wake wenye sauti nyororo ambayo ilikonga nyoyo za mashabiki mbalimbali wa Bongo Flava.

Baadhi ya nyimbo zilizomletea umaarufu mkubwa ni Nataka Niwe Wako, Mapenzi Ni Ya Wawili (Nafurahi), na Choma Choma.

Video: Maunda Zorro – Nataka Niwe Wako

Akiimba pamoja na Kaka Yake Banana Zorro

Mwenyezi Mungu Aipumzishe Roho Ya Marehemu Maunda Zorro Pema Peponi.

Previous articleUber Yasitisha Huduma Zake Za Usafiri Tanzania
Next articleRais Samia Akutana na Makamu Wa Rais Wa Marekani Kamala Harris