Uchaguzi Mkuu wa kuchagua rais wa marekani kwa kipindi cha miaka mingine minne unafanyika leo huku kukiwa na ushindani mkali kati ya mgombea wa chama cha Republican ambaye pia ni rais wa sasa, Donald J. Trump, na makamu wa rais wa zamani, Joe Biden kutoka chama cha Democratic.

Uchaguzi huu ambao umekuwa na ushindani wa hali ya juu kutokana na mgawanyiko mkubwa wa kiitikadi kwa raia wa Marekani kulikosababishwa kwa kiasi kikubwa na siasa za rais Trump.

Rais Trump ambaye aliingia madarakani kwa kumshinda Hillary Clinton mwaka 2016, amekuwa akishutumiwa vikali kwa siasa za kibaguzi, chuki dhidi ya wahamiaji kutoka mataifa yasiyo na wazungu hawa wamexico na waafrika.

Pamoja na hayo, rais Trump Donald Trump pia anashutumiwa kuhamasisha makundi mbalimbali ya kizungu yenye siasa kali zenye nia ya kuhakikisha upendeleo kwa utawala wa watu weupe nchini humo.

Hali hii imesababisha makundi mengi hasa ya wahamiaji kuhamasishana ili kuhakikisha rais Trump anatolewa madarakani kupitia sanduku la kura.

Kuna wasiwasi wa kutokea vurugu kubwa iwapo mgombea yeyote kati yao atashindwa, hali hii imesababishwa maduka na sehemu mbalimbali za biashara kujiandaa vilivyo kwa kuweka uzio wa mbao kuziba madirisha na milango ya sehemu zao za biashara.

Kwa upande wake, mshindani wa rais Trump kutoka chama cha Democtratic, makamu wa rais wa zamani wa Joe Biden, yeye ameahidi iwapo atashinda, atahakikisha analiunganisha taifa la Marekani na kupambana vilivyo na ugonjwa wa Covid-19 ambao mpaka sasa unahatarisha maisha ya wamarekani wengi kiafya na kiuchumi.

Pamoja na kuchagua rais, wamarekani pia watachagua maseneta, wawakilishi (wabunge), magavana, madiwani, na mpaka majaji wa mahakama mbalimbali.

Previous articleNviiri the Storyteller Feat. Femi One – Bar
Next articleAfrica’s week in pictures: 30 October – 5 November 2020