russia aeroflot airbus

Rais wa Urusi Vladimir Putin ametia saini sheria ambayo itaruhusu mashirika ya ndege ya Urusi kuchukua udhibiti wa mamia ya ndege zilizotengenezwa na nchi za Magharibi na kukodishwa kutoka katika makampuni mbalimbali ya ukodishaji ndege ya kimataifa, shirika la habari la Urusi TASS liliripoti.

Ndege hizo zitaongezwa kwenye orodha ya ndege za nchi hiyo na kutumiwa kwenye safari za ndani ya nchi hiyo. Habari hizo zinakuja baada ya kisiwa cha Bermuda kubatilisha vyeti vya ubora wa ndege zaidi ya 700 zilizokodishwa nchini Urusi, ambazo zilianza kutekelezwa Jumamosi usiku.

MOSCOW, RUSSIA – APRIL 21, 2014: Aeroflot Boeing-777 interior. OJSC Aeroflot – Russian Airlines is the flag carrier and largest airline of the Russian Federation

Vita kati ya Urusi na wakopeshaji imekuwa ikiendelea tangu uvamizi wa Ukraine mnamo Februari 24, huku Umoja wa Ulaya ukizilazimisha kampuni za kukodisha ndege kufuta kandarasi zao na mashirika ya ndege ya Urusi ifikapo Machi 28, hii inamaanisha kwamba ndege hizo za kigeni zinahitaji kurejeshwa kwa wamiliki wao.

Hata hivyo, serikali ya Urusi na mashirika hayo ya ndege yamefanya kazi hiyo kuwa ngumu, ikiwa ni pamoja na kufungwa kwa anga na kupiga marufuku safari nyingi za ndege za kimataifa.

Vladimir Putin of Russia

Wakati huo huo, vikwazo vya Ulaya na Marekani vimezuia ushirikiano na ufanyaji biashara kati ya mashirika ya ndege ya Urusi na makampuni makubwa ya utengenezaji ndege ya Airbus na Boeing, ambao ndio walizalisha sehemu kubwa ya ndege zilizokodishwa Urusi. Hiyo ina maana kwamba makampuni hayo mawili ya Magharibi hayawezi kutoa ushauri wa kitaalamu kwenye matengenezo, ununuaji vipuri, au marekebisho ya ndege hizo, hali hii inaweza kuleta hatari kwa abiria na wafanyakazi wa ndege hizo.

Kwa vile Boeing na Airbus zimepigwa marufuku kusafirisha vipuri kwenda Urusi, hii inaweza kulazimisha mashirika ya ndege kutafuta njia mbadala hatari, kama vile kununua bidhaa ambazo hazijaidhinishwa kutoka China au kung’oa vipuri kwenye ndege nyingine ili kufanyia matengenezo ndege zilizoharibika.

Kulingana na mshauri wa masuala ya usafiri wa anga Ishka, ndege zenye thamani ya dola bilioni 10 zimekwama nchini Urusi.

“Wakodishaji wanaweza kuishia kuzihesabu ndege hizo kama moja ya hasara ya kampuni zao,” Nick Cunningham, mchambuzi wa mambo ya ukodishaji ndege alisema.

Previous articleRais Samia Atoa Sh. Milioni 15 Kwa Taasisi Ya Ali Kimara
Next articleHarmonize – Bakhresa