Rais Samia Suluhu Hassan

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia  Suluhu Hassan ametoa Shilingi milioni 15 kwa lengo la kuisaidia Taasisi ya Ali Kimara huku akiipongeza Klabu ya Yanga kwa kuamua kucheza mchezo wa ngao ya hisani dhidi yao na timu ya Somalia.

Mtoto Ali Kimara akiwa na wazazi wake.

Mchezo huo wa kirafiki ulipigwa jumamosi hii kwenye uwanja wa Azam Complex nje ya jiji la Dar es Salaam.

Mama Samia aliipongeza Klabu hiyo ya Yanga kwa wazo hilo la kucheza mchezo wa kuchangia mfuko huo kwa ajili ya kumchangia Aly Kimara.

“Nilikuwa nawaza kufanya kama mlivyofanya ninawapongeza kwa wazo zuri la kucheza mchezo wa hisani kwa lengo la kusaidia mfuko huo ninawatakia mchezo mzuri msiumizane,alisema Mama Samia.

Kwa upande wa Taasisi ya GSM ilichangia mfuko huo kiasi cha shilingi milioni 10.

Previous articleSaudi Arabia “Yanyonga” Watu 81 Ndani Ya Siku Moja
Next articleUrusi Yapitisha Sheria Ya Kutaifisha Ndege Za Nchi Za Magharibi