Marais wa zamani wa Marekani, Bill Clinton, George W. Bush, na Barack Obama, wamejitolea kuanza kufanya chanjo ya ugonjwa wa COVID-19 unaosababishwa na virusi vya aina ya Corona.
Marais hao wameamua kujitangaza hadharani kujitolea kwao na kuchukua chanjo hiyo kama njia ya kuhamasisha wananchi wengine kutokuogopa na kuanza kufanya chanjo hiyo.
Uamuzi wa marais hao wa zamani umekuja baada ya wananchi wengi wa Marekani na nchi mbalimbali duniani kuitilia shaka chanjo hiyo kuwa ni mkakati maalumu wa baadhi ya mashirika na matajiri wakubwa duniani ili waweze kujitajirisha kibiashara.
Makampuni mawili makubwa ya madawa duniani ya Pfizer na Moderna yamewasilisha maombi kwenye Mamlaka ya Uthibiti Madawa na Chakula ya Marekani (FDA) ili chanjo zao ziweze kutumiwa na binadamu.
Ugonjwa wa COVID-19 umeendelea kuathiri nchi mbalimbali duniani na kusababisha vifo vya watu wengi hasa wazee.