Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na wenzake watatu, leo Machi 4, 2022 wamefutiwa mashtaka yote yaliyokuwa yakiwakabili katika Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi.

Hali ilivyokuwa ndani ya Mahakama Kuu baada ya Mbowe na wenzake kuachiwa huru.

Mbowe na wenzake wameachiwa baada ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali, DPP, kuwasilisha hati ya kutokuwa na nia ya kuendelea na shauri hilo.

Kesi hiyo namba 16 ya mwaka 2021 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dhidi ya Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling’wenya, na Freeman Mbowe ilitajwa leo mapema katika Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi jijini Dar Es Salaam.

Hatua hii imekuja ikiwa imepita siku moja tu baada ya viongozi mbalimbali wa dini kumtembelea Rais Samia Suluhu Hassan huku wakimuomba serikali kumfutia kesi hiyo Freeman Mbowe na wenzake.

Kesi hiyo ambayo ilikumbwa na vikwazo mbalimbali kwa upande wa serikali kutokana na kukosa ushahidi wa kutosha kwenye mashtaka yake. Maelfu ya watanzania walishaona mapungufu makubwa ya kesi hiyo dhidi ya Mbowe na wenzake.

Mbowe na wenzake walikuwa wakitetewa na jopo la mawakili 11 wakiongozwa na wakili maarufu wa Chadema Peter Kibatala.

Jopo la mawakili waliokuwa wakimtetea Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake wakitoka mahakamani huku wakiongozwa na wakili maarufu Peter Kibatala.
Previous articleRacism Claims Start To Emerge From Ukraine: Africans Are Blocked From Getting On Trains To Flee
Next articleRais Samia Akutana Na Freeman Mbowe