Ummy Mwalimu
Waziri wa Afya wa Tanzania, Mh. Ummy Mwalimu akiongea jana mjini Dodoma.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo kuanzia tarehe 17 Machi mwaka 2022, imeondoa rasmi sharti la wasafiri wote wanaoingia ambao wamechanja chanjo ya UVIKO (COVID) kuwa na cheti cha PCR ili kupima kama wana virusi vya COVID-19.

Uamuzi huo wa serikali ulitangazwa rasmi jana na Waziri wa Afya, Mh. Ummy Mwalimu mjini Dodoma. Ulegezaji wa masharti haya kwa wasafiri hauwahusu wale wote ambao mpaka hivi sasa bado hawajachanjwa.

Waziri Ummy Mwalimu amesema kutokana na kupungua kwa maambukizi duniani, Serikali imelegeza masharti ya wasafiri wanaoingia nchini ambapo kunaondolewa hitaji la kuwa na cheti cha kipimo (Negative RT-PCR Certificate) kilichokuwa kikihitajika kwa kila msafiri anayeingia Tanzania hapo awali.

Previous articleHarmonize – Bakhresa
Next articleMaadhimisho Ya Mwaka Mmoja Tangu Rais Magufuli Afariki Dunia