
Leo ni maadhimisho ya mwaka mmoja tangu Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Joseph Magufuli afariki dunia. Maadhimisho hayo yanafanyika mkoani Geita katika wilaya ya Chato.


Maadhimisho hayo yatahudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais, Dkt. Isdori Mpango, Waziri Mkuu, Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa.


Viongozi wengine watakaoshiriki katika maadhimisho hayo ni Spika wa Bunge la Tanzania, Dkt. Tulia Ackson, Jaji Mkuu, Profesa Ibrahim Juma, Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi na viongozi wengine mbalimbali wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
