Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza katika kikao na Watanzania wanaoishi nchini Ubelgiji na Luxembourg leo tarehe 18 Februari, 2022 Brussels nchini Ubelgiji.

Rais Samia ambaye yuko barani ulaya akihudhuria vikao mbalimbali na kukutana na viongozi wa taasisi mbalimbali za kimataifa.

Katika mkutano wake huo na Watanzania hao wa diaspora, Rais Samia alitoa ahadi kuwa serikali yake, itapeleka muswada bungeni kwa ajili ya kutoa hadhi maalum kwa Watanzania wa diaspora.

Previous articleFreeman Mbowe Na Wenzake Wakutwa Na Kesi Ya Kujibu
Next articleRussia Attacks Ukraine: Explosions In Kyiv