
Mahakama Kuu Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi leo Februari 18, 2022 imetoa uamuzi kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe pamoja na Washtakiwa wengine watatu wana Kesi ya Kujibu.

Jaji Tiganga alitoa uamuzi huo leo mapema wakati wa usikilizwaji wa keshi hiyo katika Mahakama Kuu ya Uhujumu Uchumi na Rushwa jijini Dar Es Salaam huku mamia ya wananchama na wapenzi wa Chadema wakiwa kwenye eneo hilo la mahakama.

Kesi hiyo imeahirishwa mpaka tarehe 4 Machi, 2022.