Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amekutana leo na kufanya mazungumzo mafupi na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mhe. Tundu Lissu.
Mazungumzo hayo yamefanyika baada ya Rais Samia ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kukubali maombi ya kiongozi huyo wa Chadema kukutana naye na kuzungumza jijini Brussels nchini Ubelgiji.
Aidha katika mazungumzo hayo Mhe. Rais na Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu, walizungumza masuala mbalimbali yenye maslahi na ustawi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mhe. Tundu Lissu, alikuwa mgombea wa Urais katika uchaguzi mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 2015 kupitia Chadema.