MWENYEKITI wa Klabu ya Simba Al Murtaza Mangungu amesema amefurahishwa na kiwango kilichoonyeshwa na wachezaji  wao katika mchezo wa Kombe la Shirikisho  hatua ya Makundi dhidi ya timu ya Asec Mimosas  ya nchini Ivory Coast.

Akizungumza jijini baada ya mchezo huo Mangungu alisema timu yao imefanikiwa kupata ushindi licha ya kupoteza nafasi nyingi.

“Tunashukuru timu yetu imefanya vizuri katika mchezo huo mikakati yetu ni kufanya vizuri kwenye mashindano ya Kimataifa, alisema Mangungu.

Mwenyekiti huyo aliongeza kuwa baada ya ushindi huo wiki hii wanatarajia kuelekea nchini Morocco kukutana na timu ya RS Bercane,na kudai hakuna timu yoyote wanayoihofia kwenye kundi lao.

“Hatuhofii kucheza na timu yoyote kwa kuwa kikosi chetu kipo imara pande zote tunawashukuru watanzania kwa umoja waliotuonyesha, alisema.

Naye Kocha mkuu wa Klabu hiyo Pablo Franco aliwapongeza wachezaji kutokana na kiwango hicho. Pablo alisema wachezaji wake walitumia vizuri maelekezo aliyowapa na kuleta sura mpya ya matokeo.

“Ninafurahi kwa sababu nimepata faida ya ushindi kwenye uwanja wa nyumbani ninaahidi kujipanga kwa ajili ya mchezo ujao, alisema Franco.

Simba iliifunga timu ya Asec Mimosas mabao  3-1.

Previous articleRais Samia Atoa Bilioni 1.5 Kuuinua Mfuko Wa Wasanii
Next articleRais Samia Suluhu Hassan Akutana na Tundu Lissu Nchini Ubelgiji