Wajumbe wa Bunge la Ulaya wakiongozwa na mwenyekiti wa kamati ya mambo ya nje ya Bunge la Umoja wa Ulaya, David McAllister, wamehoji ni vigezo gani vilivyotumika kutoa ahadi ya msaada wa Euro Milioni 27 za kusaidia kupambana na gonjwa la COVID-19 kwa serikali ya Tanzania iliyotolewa na Rais wa Baraza la Umoja wa Ulaya, Charles Michel.

Mwenyekiti wa kamati hiyo ametoa maelekezo kwa Umoja wa Ulaya sasa iiangalie Tanzania kwa jicho makini zaidi na kufuatilia kwa umakini juu ya hali ya kutisha ya ukandamizwaji wa haki za binadamu na utawala bora kunakoendelea Tanzania chini ya utawala wa Rais John Magufuli.

Mwenyekiti huyo wa kamati ya mambo ya nje ya Umoja huo wa Ulaya, David McAllister, anaiwakilisha Ujerumani kwenye Umoja huo.

Wabunge hao waliendelea kuhoji kwanini Umoja huo ulitoa ahadi ya fedha kiasi cha Euro Mil. 27 (Zaidi ya Tsh. Bilioni 74) za kusaidia harakati za kupambana na Coronavirus hasa ugonjwa wa COVID-19.

Wakiongozwa na mwenyekiti wa kamati ya mambo ya nje ya Umoja huo, D. McAllster, wabunge hao walimbana kwa kumhoji ofisa wa Umoja huo kuhusu vigezo gani vilitumika kuona Tanzania inastahili kupewa msaada huo wakati haifuati maelekezo ya Shirika la Afya Duniani (WHO) na na huku serikali ya Tanzania ikiwa wameshatangaza kuwa nchi iko huru dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona vinavyosababisha gonjwa hilo.

Wabunge hao Wamesema sasa Umoja huo uangalie kwa namna gani watatoa msaada wao na fedha zao kwa vyama vya siasa vinavyotetea demokrasia na watetezi wa haki za binadamu waliopo Tanzania na sio kutoa tena fedha kwa Serikali iliyo madarakani.

Sintofahamu hii imekuja baada ya uchaguzi mkuu wa Tanzania kwa mwaka 2020 kulalamikiwa na vyama vya upinzani na mataifa mengine ya ulaya na Marekani kuwa haukuwa huru na haki.

Mapendekezo mengine yalitolewa na wabunge hao ni kukata misaada ya kibajeti kwa serikali ya Tanzania. Umoja ni mmoja ya wadau wakubwa wa kimaendeleo kwa serikali ya Tanzania.

Mgawanyo wa misaada ya Umoja wa Ulaya kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na vigezo mbalimbali inavyobidi vifuatwe kufanikisha misaada hiyo.

Uchaguzi huu umerudisha tena madarakani kwa mingine mitano, utawala wa Rais John Magufuli, huku wagombea ubunge wa chama tawala, Chama Cha Mapinduzi (CCM), wakijizolea karibu viti vyote vya ubunge na uwakilishi.

Previous articleNandy Feat. AliKiba – Nibakishie
Next article37 Die In A Violent Start To Uganda’s Election Season