Kufuatia kifo cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais, Mh. Samia Suluhu Hassan ataapishwa kuwa Rais mpya wa Tanzania Machi 19, 2021 kuanzia saa 4 asubuhi Ikulu jijini Dar Es Salaam.
Mh. Samia Suluhu alizaliwa mwaka 1960 katika kisiwa cha Zanzibar, huku elimu yake akiipatia Tanzania na baadae kupata elimu ya juu Machester University nchini Uingereza akisomea masuala ya uongozi wa jamii, kwa hivi sasa ana umri wa miaka 61.
Hii itakuwa mara ya kwanza kwa Tanzania kuongozwa na Rais mwanamke, na pia atakuwa mmoja kati ya marais wachache wananwake Afrika na duniani.
Aliolewa mwaka 1978 na Hafidh Ameir na kwa pamoja wana watoto wanne. Mmoja wa watoto wake, Mwanu Hafidh Ameir, ni mjumbe wa baraza la kuu la Wawakilishi Zanzibar.
Samia Suluhu atakuwa rais wa tisa mwanamke kuwahi kushika madaraka ya urais barani Afrika toka nchi za kiafrika zipate uhuru na mmoja kati ya marais wachache wanawake duniani.