Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. John Magufuli, amewapigia magoti wananchi wa mji wa Njombe mkoani Iringa ambao walijitokeza kumsikiliza kwenye mkutano wake wa kampeni za uchaguzi mkuu wa Tanzania.

Rais Magufuli huku akiwa na viongozi wengine wa Chama Cha Mapinduzi, alionekana akipiga magoti huku akiombewa kura kutoka kwa mmoja wa viongozi wa CCM wa mkoa huo kama ishara ya unyenyekevu kwa wananchi hao.

Uchaguzi mkuu wa mwaka huu wa 2020 umekuwa na ushindani mkubwa kwenye kampeni kutokana na mgombea kutoka upinzani wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Tundu Lissu, kuwa anakusanya maelfu ya Watanzania kwenye mikutano yake mbalimbali ya kampeni.

Mgombea wa CHADEMA, Tundu Lissu, anajaribu kuomba ridhaa ya Watanzania kwenye nafasi ya Urais ili kumtoa madarakani Rais John Magufuli na Chama Cha Mapinduzi ambacho kimekuwa madarakani kwa muda mrefu.

Uchaguzi mkuu ambao unafanyika tarehe 28 Oktoba, unaonekana utaleta ushindani mkubwa dhidi ya Chama Cha Mapinduzi kuliko kipindi kingine chochote toka siasa za vyama vingi zilipoanzishwa Tanzania.

Previous articleZuchu Feat. Diamond Platnumz – Litawachoma
Next articleTume Ya Taifa Ya Uchaguzi Tanzania Yamfungia Tundu Lissu Kufanya Kampeni Za Urais