Tume ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania (NEC) imemfungia mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia Na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu kwa siku saba kwa madai ya kukiuka maadili ya kukiuka maadili ya Uchaguzi.
Kulingana na taarifa iliyotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi, inaonyesha kamati ya maadili ya tume hiyo kitaifa imesikiliza malalamiko dhidi ya mgombea wa kiti cha urais kupitia CHADEMA Bwana Tundu Lissu.
Malalamiko yaliwasilishwa na Chama cha NRA na Chama cha Mapinduzi. Chama cha NRA walilalamikia kitendo cha mgombea wa kiti cha Rais kupitia CHADEMA kutoa maneno ya uchochezi yasiyothibitika. Ambapo akiwa mkoani Mara, alisema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano, Mhe. John Pombe Magufuli ameitisha kikao cha wasimamizi wa Uchaguzi nchi nzima ili kuhujumu uchaguzi. Pia imeelezwa kuwa alitoa maneno ya kichochezi na ya kudhalilisha kinyume na Maadili ya Uchaguzi akiwa mkoani Geita.
Barua ya kumtaka kujibu tuhuma hizo iliwasilishwa kwa Katibu mkuu wa CHADEMA kwa mujibu wa taratibu. Katibu Mkuu wa CHADEMA alijibu kuwa, malalamiko hayakihusu chama hivyo, mgombea na chama ni vitu viwili tofauti. Pamoja na kwamba Katibu mkuu wa CHADEMA alijibu barua ya malalamiko kuwa malalamiko apelekewe Tundu Lissu mwenyewe, kamati ya maadili imeridhika kuwa taarifa kuhusu malalamiko ya ukiukwaji na Maadili iliwasilishwa kwa mlalamikiwa kwa mujibu wa taratibu kwa kuzingatia masharti ya ibara ya 39 ya Katiba ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ambapo bwana Tundu Lissu alidhaminiwa na CHADEMA kugombea kiti cha Rais. Hivyo, barua ya malalamiko kuwasilishwa kwa Katibu Mkuu ni sahihi kabisa.
Hivi karibuni mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Dkt. Wilson Mahera, alionekana akitoa hoja zilizoashiria na kuaminika na wengi kuwa ni njia yake kuipigia kampeni CCM na mgombea wake, Dkt. John Magufuli. Zoja hizo ambazo hazikufaa kutolewa na mkurugenzi wa uchaguzi ambaye anatakiwa asiwe upande wa chama chochote.