Zaidi ya mwezi mmoja umeshapita tangu nchi ya Urusi ilipoivamia Ukraine. Mji wa Mariupol umeachwa ukiwa umeharibiwa vibaya, kama inavyoonyeshwa kwenye picha, mji huu wenye bandari umefanyiwa uharibifu mkubwa uliosababishwa na mashambulizi yanayoendelea kutoka kwa jeshi la Urusi.
Kabla ya vita, Mariupol ulikuwa mji wa 10 kwa ukubwa nchini humo, wenye wakazi zaidi ya 430,000. Lilikuwa jiji kuu la kisasa lililojaa sanaa na utamaduni. Ukumbi wa Drama ya Mkoa wa Donetsk, viunga vichache kaskazini mwa Bahari ya Azov katikati mwa jiji, ulikuwa mojawapo ya alama zake nyingi.
Angalia picha za hapo chini zinavyoonyesha jinsi mji ulivyokuwa na mandhari nzuri kabla ya uvamizi wa Urusi.
Lakini mashambulizi ya mara kwa mara ya vikosi vya Urusi – zaidi ya mashambulizi 50 hadi 100 kwa siku ya nchi kavu, angani na baharini – yamesababisha mamia kwa maelfu kuukimbia mji huo, maafisa wa Ukraine walisema.
Meya wa Mariupol, Vadym Boichenko, hivi majuzi alitoa wito kwa watu waliosalia, ambao alikadiria kuwa watu 160,000, kuondoka kikamilifu katika jiji hilo ambalo limezingirwa. Ofisi yake ilisema wiki hii kwamba karibu 5,000 ya wakaazi wameuawa, ikiwa ni pamoja na zaidi ya watoto 200.
Wakazi wote waliobaki katika mji huo mpaka hivi sasa hawana chakula, maji, na umeme.