Rais wa Zanzibar, Hussein Mwinyi ametangaza kifo cha Maalim Seif Sharif Hamad, Makamu wa Kwanza wa Rais aliyefariki leo Jumatano saa 5:00 asubuhi, Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam.
Serikali imetangaza siku 7 za maombolezo ambapo bendera zitapepea nusu mlingoti. Maalim Seif atakumbukwa kwa harakati zake za kutetea haki za Zanzibar na Wazanzibari na ameshakuwa mgombea wa kiti cha urais Zanzibar mara kadhaa kupitia Chama Cha Wananchi (CUF) na mara ya mwisho kwenye uchaguzi wa mwaka 2020 kwa kupitia Chama Cha ACT Wazalendo.
“Taarifa za msiba na maziko zitaendea kutolewa na serikali kwa ushikiriano karibu na familia pamoja na Chama cha ACT Wazalendo.”
Mwenyezi Mungu ampumzishe kwa amani Maalim Seif Sharif Hamad.