Msanii wa Bongo Flava Baby Madaha

Msanii wa bongo flava, Baby Madaha hivi karibuni amezungumzia yaliyojiri kati yake na msanii mwenzake ajulikanae kama Juma Nature baada ya wawili hao kuonekana kuwa na ukaribu uliopitiliza.

Kama ilivyozoeleka kibongobongo watu wawili wenye jinsia tofauti wakiwa karibu, huwa kunajambo kati yao. Madaha akiongea na Bongo Radio hivi karibuni, alifunguka ya kwamba yeye na Juma Nature hawakuwai kuwa na uhusiano wa kimapenzi kama inavyodhaniwa na watu wengi.

Madaha alieleza kwamba ukaribu uliokuwepo kati yao ni kutokana na kazi ya muziki, kwani kwa mujibu wa Madaha, Juma Nature alikua akimpa mawazo na miongozo ya sanaa ya muziki. Lakini pia Madaha aliongeza kwa kusema kwamba, Nature alimfundisha maisha kwa kiasi kikubwa. “Nature alinifundisha maisha, kwani nilikua na akili za kitoto sana, na nilikua na complicate maisha, Nature alinifundisha kupanda Daladala na bodaboda pia”. Alisema.

Baby Madaha akitumbuiza katika moja ya matamasha yake

Madaha alisema kwamba Nature alikua na ndoa yake na yeye aliliheshimu jambo hilo, lakini mpaka sasa hana uhakika kama ndoa ya Nature bado ipo hai au laa. Aliongeza kwa kusema kuwa, sasa hivi yeye yupo kwenye mahusiano yake na anataka mashabiki waelewe hivyo kuwa hakuna kinachoendelea kati yake na Juma Nature.

Akizungumzia  ukimya wake katika muziki, anasema kwamba ni kutokana na mikataba iliyokua ikimkwaza kati yake na usimamizi alioupata Nchini Kenya. Lakini pia kutokana na kushindwana na meneja wake nchini kenya, aliamua kuvunja mkataba na kurejea Bongo.

Madaha anaeleza kwa sasa ameshaachia ngoma mpya iitwayo UMENIKOROGA, lakini pia amedai hivi karibuni ataandaa kitu kwa ajili ya valentine, hivyo mashabiki wake wakae tayari.

Baby Madaha katika pozz.

Akitoa mtazamo kuhusu tasnia ya muziki wa Bongo Flava, anaeleza kua tasnia inazidi kukua siku hadi siku na inaelekea pazuri zaidi, japokua kuna changamoto ambazo haina budi kukabiliana nazo. Madaha anamalizia kwa kusema kwamba wasanii wanatakiwa kuachana na matumizi ya madawa ya kulevya, kwani madawa hayo sio kitu cha kukimbilia kutokana na ukweli kwamba, tasnia imeshapoteza wasanii kadhaa kutokana na matumizi ya madawa hayo.

Previous articleIjue Hifadhi Ya Taifa Ya Serengeti Nchini Tanzania
Next articleMakamu Wa Kwanza Wa Rais Zanzibar Maalim Seif Afariki Dunia