Serengeti ni hifadhi kongwe, lakini pia ni hifadhi maarufu sana duniani kote inayopatikana nchini Tanzania. Inatajwa kuwa ni urithi wa dunia, hifadhi hii inaongoza kwa umaarufu duniani na ina ukubwa wa kilomita za mraba zipatazo 14,763 na ndio hifadhi ya pili kwa ukubwa barani afrika ikifuatiwa na hifadhi ya Kruger nchini afrika ya kusini. Wanyamapori zaidi ya milioni tatu wanapatikana ndani ya hifadhi hii.

Moja kati ya mambo yayayoipatia umaarufu hifadhi hii ni pamoja na misururu ya nyumbu wapatao zaidi ya miloni moja wanao hama kutoka upande mmoja wa hifadhi na kuvuka mpaka wa Tanzania wakielekea Pori la akiba la Maasai Mara nchini Kenya.

Nyumbu wakivuka mto Mara wakati wa Great Migration.

Misafara ya nyumbu hawa hufikia urefu wa kilometa 40 kati ya wale nyumbu wa mwanzo hadi wa mwisho. Nyumbu hawa hutembea umbali wa kilometa 1000 wakati wa kuhama. Huu pia ndio huwa wakati wa kuzaliana ambapo kiasi cha ndama 8000 huzaliwa kwa siku.

Maelfu ya wanyama hawa huuawa na kuliwa na wanyama wengine kama vile simba na mamba wakubwa wanaoishi ndani ya mto Mara. Hifadhi hii ya Serengeti pia ina idadi kubwa ya Simba na Duma, lakini pia Serengeti ina mandhari nzuri ya asili hasa uwanda mpana uliojaa majani na mawe yaitwayo Kopje ambayo kwa pamoja huleta sura ya asili ya dunia kabla ya kuumbwa kwa mwanadamu.

Maelfu ya Nyumbu wakihama kuelekea hifadhi ya Maasai Mara nchini Kenya.

Pichani Mamba wakimshambulia Nyumbu ndani ya mto Mara.

Hifadhi hii ipo umbali wa kilometa 335 kutoka Arusha mjini, pia inaweza kufikika kupitia miji ya Musoma na Mwanza. Wakati mzuri wa kutembelea hifadhi hii ni kuanzia mwezi Juni hadi Disemba baada ya mvua za masika, ambapo wanyama karibu wote huonekana kwa urahisi zaidi.

Pichani Simba wakimshambulia Nyumbu ndani ya Hifadhi ya Serengeti.

Wanyama wengine wanaopatikana ndani ya hifadhi hii ni Pundamilia zaidi ya 200,000, Swala zaidi ya 300,000, Tembo, Fisi, Mbwamwitu, Mbweha na Nyani.

Watalii wakitazama wanyama hifadhini Serengeti.

Huduma za malazi zinapatikana ndani ya hifadhi, kwani kuna lodge mbalimbali kwa ajili ya kutoa huduma za malazi na chakula kwa wageni wanaotembelea hifadhi. Mbali ya uwepo wa Lodge, lakini pia kuna Makambi ya wageni (Tented Camps) ambazo pia hutoa huduma kwa wageni.

Watalii wakiangalia wanyama wanapovuka mtoni wakati wa Great Migration ndani ya hifadhi ya Serengeti.

Hifadhi hii imetangazwa na kituo cha Televisheni cha ABC cha nchini Marekani pamoja na gazeti la kila siku la USA Today kuwa ni ajabu saba la dunia.

Previous articleTambua Historia Ya Bi Kidude Malkia Wa Taarab Zanzibar
Next articleBaby Madaha Aweka Wazi Kati Yake Na Juma Nature