Leo siku ya tarehe 28 Oktoba, 2020, ni siku ya uchaguzi mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Siku ya leo watanzania watapata fursa ya kuchagua Rais na Makamu wake wa Tanzania. Pia kwa upande wa Zanzibar, watachagua Rais Wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza La Mapinduzi.

Jumla ya wagombea 15 kutoka vyama mbalimbali 15 wamejitokeza kugombea nafasi ya Urais wa Tanzania. Pamoja na wingi wa wagombea wote hao, ushindani mkubwa uko kati ya mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu na Rais wa sasa wa Tanzania akiwakilisha Chama cha Mapinduzi (CCM), John Magufuli.

Wagombea wa nafasi ya Urais wa Tanzania wakiwakilisha vyama vya siasa 15 nchini Tanzania.

Kwa takribani miezi miwili, wagombea hao wawili na wengine kutoka vyama 13, wamezunguka sehemu mbalimbali nchini Tanzania huku wakinadi sera zao na kuomba ridhaa ya kupewa miaka mitano ya uongozi kutoka kwa Watanzania.

Rais John Magufuli na Tundu Lissu waliweza kujaza umati wa watu kila kona ya nchi waliyotembelea kunadi sera zao na za vyama vyao. Mgombea wa CHADEMA alipokelewa na umati mkubwa wa watyu karibu kila sehemu aliyotembea pamoja na vikwazo mbalimbali alivyokutana navyo wakati wa uchaguzi.

Kwa upande wa Zanzibar, Maalim Seif ambate ni mgombea wa kiti cha urais kwa ACT Wazalendo, na Hussein Mwinyi ambaye ni mkombea wa kiti cha urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) walitia fora kwa kujaza umati wa watu kwenye mikutano yao.

Tafadhali tutegee sikio, kwani tutakuwa tunawaletea matokea moja kwa moja kutokea makao makuu ya Tume ya Uchaguzi, jijini Dar Es Salaam, Tanzania.

Kwa niaba ya wote ndani ya Bongo Radio, tunawatakia Watanzania uchaguzi wa amani na utulivu.

Previous articleZanzibar Opposition Leader Says 10 killed On Eve Of Tense Election
Next articleMwenyekiti Wa CHADEMA Freeman Mbowe Ashindwa Ubunge Uchaguzi Jimbo La Hai