Rais Magufuli akila kiapo cha urais kwa miaka mingine mitano.

Rais John Magufuli, na Makamu wake Samia Suluhu, waliapishwa na jaji mkuu wa mahakama kuu ya Tanzania, Ibrahim Juma kuongoza Tanzania katika kipindi kingine cha miaka mitano. Rais Magufuli alikula kiapo akiwa ameshikilia Biblia Takatifu huku Makamu wake, Samia Suluhu, akitumia Msahafu Tukufu.

Rais Magufuli ambaye alitangazwa na tume ya taifa ya uchaguzi Tanzania (NEC) kushinda uchaguzi kwa asilimia 84%. Uchaguzi huo unalalamikiwa na vyama vya upinzani na jumuiya za kimataifa kuwa haukuwa huru na wa haki.

Malalamiko hayo ya vyama vya upinzani vikiongozwa na CHADEMA na ACT Wazalendo kuhusiana na uchaguzi, yamepelekea kuvifanya viitishe maandamano ya amani nchi nzima. Maandamano hayo ambayo hayajafanikiwa kufanyika kutokana na viongozi wakuu wa vyama hivyo kukamatwa na jeshi la Polisi.

Na pia kuna habari kuwa mgombea Urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, ameomba hifadhi kwenye ubalozi wa Ujerumani nchini Tanzania akihofia usalama wa maisha wake. Ikumbukwe Mh. Lissu alirudi nyumbani Tanzania akitokea Ubelgiji alipokuwepo kwa matibabu kutokana na kupigwa risasi 16 mjini Dodoma wakati wa vikao vya bunge mwaka 2017.

Previous articleAfrica’s week in pictures: 30 October – 5 November 2020
Next articleKelly Rowland And More Celebrities Who Are Expecting In 2021