
Rais mteule wa Marekani, Joe Biden, ameahidi kuindoa Tanzania na nchi nyingine za Kiafrika kwenye orodha ya nchi zilizowekewa vikwazo vya kusafiri nchini Marekani ambavyo viliwekwa na rais anayemaliza muda wake kutokana na kushindwa uchaguzi wa mwezi Novemba, Donald J. Trump.
Joe Biden ameahidi kuviondoa vikwazo hivyo ndani ya siku ya kwanza baada ya kuapishwa urais mnamo tarehe 20 Januari 2021. Ahadi hiyo ni moja ya kati ya ahadi nyingi mgombea huyo urais wa Marekani aliziweka wakati wa kampeni za uchaguzi uliomuondoa madarakani Rais Donald J. Trump.

Kwenye orodha hiyo ambayo Tanzania ilikuwa hairuhusiwi kushiriki kwenye bahati nasibu ya kuhamia Marekani au kama inavyojulikana kwa jina maarufu la “Green Card Lottery”
Nchi nyingine ambazo nazo ziliwekewa vikwazo mbalimbali vya kuingia nchini Marekani na serikali ya rais Donald Trump ni Iran, Libya, Somalia, Syria, Yemen, Venezuela, North Korea, Nigeria, Myanmar, Eritrea, Kyrgyzstan, na Sudan.
Wanaharakati wengi wamedai vikwazo hivi viliwekwa na serikali ya Trump kutokana na ubaguzi wake dhidi ya watu weusi na Waislamu.
Rais Trump ambaye mpaka hivi sasa amegoma kuyakubali matokeo ya kushindwa kwake urais kwenye uchaguzi mkuu, anatarajiwa kumpisha rais mteule, Joe Biden ndani ya Ikulu ya Marekani kuanzia siku ya tarehe 20 Januari 2021.