Mchezaji wa soka wa kimataifa wa Kitanzania, Mbwana Ally Samatta, amehamia timu ya Fenerbahce ya nchini Uturuki akitokea timu ya Aston Villa nchini Uingereza. Mbwana ambaye PIA alihamia timu ya Aston Villa mwezi January mwaka huu akitokea nchini Ubelgiji alipokuwa akichezea timu ya Genk.

Mchezaji huyu ambaye anahamia timu ya Fenerbahce kwa mkopo wa msimu mzima. Timu hiyo imeingia mkataba na Mbwana Samatta aweze kuichezea kwa jumla ya miaka minne. Mkopo huo ambao utaigharimu timu ya Fenerbahce kati ya paundi milioni ÂŁ5.5m mpaka ÂŁ6.2m.

Mbwana Ally Samatta akitambulishwa katika timu ya Fenerbahce ya nchini Uturuki.

Katika kipindi cha takribani miezi 9 ambapo amekuwa akiichezea timu ya Aston Villa, Mbwana Samatta ameweza kucheza mechi 16 huku akiifungia timu hiyo kutoka jiji la Birmingham nchini Uingereza jumla ya magoli mawili chini ya kocha Dean Smith.

Mbwana Ally Samatta

Timu ya Aston Villa ambayo mmoja wa wamiliki wake raia wa nchi ya Misri, bilionea Nassef Sawiris ambaye anakadiriwa kuwa na utajiri wa dola bilioni $7.5b.

Previous articleCovid-19 Models Predicted Devastation in Africa — But ‘The Reality is Starkly Different’
Next articleUS Federal Judge Postpones Trump Ban On Popular App TikTok