Krasukha-4

Vikosi vya kijeshi vya Ukraine vimekamata sehemu ya moja ya mifumo ya juu zaidi ya vita vya kielektroniki vya Urusi, ambayo inaweza kufichua siri zake za kijeshi.

Moduli ya komandi ya Krasukha-4 ilipatikana ikiwa imetelekezwa nje kidogo ya mji wa Kyiv ukiwa umeharibiwa kwa kiasi lakini ambao unaweza kutumika.

Picha zilizochapishwa kwenye mitandao ya kijamii zinaonekana kuonyesha kontena lililokuwa na moduli iliyofunikwa kwenye matawi ya miti, ikiwezekana katika jaribio la haraka la kuficha ili vikosi vya Urusi vikimbie mashambulizi.

Mfumo huo umeundwa kuunganisha satelaiti za obiti ya chini, ndege zisizo na rubani na makombora, lakini pia inaaminika kuwa na uwezo wa kufuatilia ndege za NATO.

Krasukha-4 kamili ni mfumo wa sehemu mbili unaojumuisha moduli ya komandi na mfumo wa vita vya elektroniki, ambao hufungwa kwenye malori ya kijeshi mawili.

Inaaminika kuwa mfumo wa Krasukha-4 ulitumiwa dhidi ya ndege zisizo na rubani za Bayraktar TB2 za Uturuki nchini Syria, ambapo zilisababisha ndege hizo nyingi kuangushwa.

Ndege hizo zisizo na rubani za Bayraktar TB2 ni miongoni mwa zile zinazotumiwa na vikosi vya Ukraine kuharibu vifaru vya Urusi, silaha na misafara ya malori ya kijeshi.

Kifaa hicho kilichokamatwa kitachunguzwa na mashirika ya kijasusi ya nchi za Magharibi na kuongeza kuwa kuna uwezekano kikachukuliwa kwa njia ya barabara hadi kambi ya jeshi la anga ya Marekani ya Ramstein nchini Ujerumani, kabla ya kusafirishwa hadi Marekani kwa uchunguzi zaidi.

Uchunguzi wa mfumo huo unaweza kufichua siri za jinsi unavyofanya kazi, ambayo inaweza kusaidia Ukraine na washirika wa Magharibi kukifanya kiharibiwe vitani.

Justin Crump, mkongwe wa kijeshi na Mkurugenzi Mtendaji wa mshauri wa uchambuzi wa hatari Sibylline, aliwaambia waandishi wa habari kwamba utekaji nyara huo ulikuwa kati ya “zawadi nyingi ambazo zimepatikana kwenye uwanja wa vita.”

“Inaonyesha jinsi mapigano yalivyotawanyika sehemu mbalimbali na ukosefu wa mawasiliano kwa upande wa Urusi,” Crump alisema.

Previous articleRais Samia Azindua Daraja La Tanzanite Jijini Dar Es Salaam
Next articleWill Smith Ampiga Kibao Chris Rock Stejini Kwenye Tuzo Za Oscars