Will Smith hit Chris Rock at the Oscars

Mcheza filamu maarufu duniani Will Smith, amempiga kibao mcheza filamu mwenzake ambaye pia ni mchekeshaji, Chris Rock, stejini katika sherehe za tuzo za 94 za Oscars jijini Los Angeles nchini Marekani.

Tuko hilo ambalo liliwashangaza watu wengi sehemu mbalimbali duniani lilitokea baada ya Chris Rock kumtania mke wa Will Smith ambaye nae pia ni mcheza filamu, Jada Pinkett Smith.

Will Smith akiwa amekaa na mkewe Jada Pinkett Smith kwenye sherehe za tuzo za 94 za Oscars jijini Los Angeles nchini Marekani.

Utani huo ulihusiana na kitendo cha Jada Pinkett kunyoa nywele zake kutokana na kuugua ugonjwa wa Alopecia, ambao humsababishia mgonjwa kupoteza nywele.

Pamoja na tukio hilo, Will Smith aliweza kushinda tuzo yake ya kwanza ya Oscar ya Muigizaji Bora kupitia filamu ya King Richard, ambapo aliigiza kama Baba wa wacheza Tennis maarufu duniani, Serena na Venus Williams.

Will Smith akiongea wakati wa kupokea tuzo ya Muigizaji Bora kwenye sherehe za tuzo za Oscars nchini Marekani.
Previous articleUkraine Yakamata Mfumo Wa Juu Zaidi Wa Kijeshi Wa Urusi Wa Vita Vya Kielektroniki
Next articleStandout Looks From The Oscars 2022 Red Carpet