RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amezindua rasmi daraja la Tanzanite jijini Dar Es Salaam lenye urefu wa Km 1.03 na upana wa mita 2.3.

Akizungumza katika hafla hiyo alisema daraja hilo limejengwa kwa gharama na kuwataka watanzania kuwa makini na miundo mbinu ya nchi.

Mwonekano tofauti wa Daraja la Tanzanite jijini Dar Es Salaam, Tanzania

Daraja hilo ambalo lina njia nne lilizinduliwa hapo jana katika hafla iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa dini pamoja na serikali.

“Leo ninazindua daraja hili la Tanzanite nikiwa naendeleza kazi aliyoiacha hayati Dokta John Pombe Magufuli ikiwemo kumuenzi pia Rais Magufuli”, alisema Rais  Samia.

Alisema daraja hilo limewekwa ulinzi wa kutosha ili kuhakikisha kila anayekwenda kwa nia mbaya anaonekana na kukamatwa haraka kupitia camera zilizowekwa.

Aliwataka viongozi wa serikali kuhakikisha wanasimamia ulinzi ikiwemo usafi wa kutosha kwenye daraja hilo ambalo hapo baadae litawekwa sanamu ya Tanzanite.

Aidha alisisitiza watu kujiandikisha kwenye zoezi la sensa ikiwemo anuani ya makazi linalotarajiwa kuanza mwezi June mwaka huu.

Naye mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makala, alipendekeza baadhi ya miradi ipewe jina la mama Samia, ili na yeye aingizwe kwenye kumbukumbu.

Alisema amelazimika kutoa kauli hiyo baada ya kufurahishwa na kazi anazozifanya Rais  Samia ndani ya mwaka wake mmoja akiwa madarakani.

Mandhari nzuri ya daraja la Tanzanite wakati wa usiku.

“Ningependekeza katika miradi ambayo Rais wetu ataizindua mmoja kati ya miradi ipewe jina la Mama Samia na yeye aingizwe katika kumbukumbu, alisema Makala.

Daraja hilo limejengwa na wakandarasi kutoka nchi ya Korea.

Previous articleNatacha – LAMOTO
Next articleUkraine Yakamata Mfumo Wa Juu Zaidi Wa Kijeshi Wa Urusi Wa Vita Vya Kielektroniki