Kwa mara ya kwanza tangu aondoke madarakani January 2020, Rais wa zamani wa Marekani, Barack Obama, alitembelea Ikulu ya Marekani iliyopo Washington, D.C. na kukutana na Rais Joe Biden.
Obama alitembea Ikulu kusherehekea utiaji sahihi wa muendelezo wa sheria aliyoianzisha wakati akiwa Rais inayohusiana na utoaji wa bima ya afya au kama inavyojulikana “Obamacare”. Sheria hiyo ya utoaji huduma za afya kwa ya bei nafuu, inawanufainisha mamia ya wamarekani wenye kipato cha chini ambao mwanzoni hawakuwa na bima ya afya. Rais Biden alikuwa makamu wa rais wa Obama kwa miaka minane.
Wakizungumza kwenye hafla hiyo, Biden na Obama walitangaza hatua ambazo Ikulu ya White House ilisema zitafanya huduma ya afya iwe nafuu zaidi, ikiwa ni pamoja na kuziba mwanya unaozuia mamilioni ya Wamarekani kufuzu kwa ruzuku.
“Ninajisikia furaha kurejea katika Ikulu ya White House. Ni muda umepita, “Obama alisema alianza matamshi yake. “Ninakiri nilisikia baadhi ya mabadiliko yamefanywa na Rais wa sasa tangu nikiwa hapa mara ya mwisho.”