Mabilionea tajiri zaidi 15 barani Afrika wamepata utajiri wao kwa kuwekeza katika tasnia kama almasi, mafuta, na biashara za bidhaa za kawaida. Kwa jumla, wana utajiri unaofikia dola bilioni $73.3, huku Aliko Dangote, tajiri mkubwa zaidi Afrika Magharibi, akiwa wa kwanza na jumla ya utajiri wa dola bilioni $13.5.
Tajiri mwingine kwenye orodha hii ni pamoja na Patrice Motsepe, mmoja wa watu matajiri zaidi nchini Afrika Kusini na mwenye utajiri unaofikia dola $2.2 bilioni. Patrice Motsepe alikuwa Mwafrika mweusi wa kwanza kutokea kwenye orodha ya mabilionea kwenye gazeti la Forbes mnamo 2008.
Pia kwenye orodha hii kuna Isabel dos Santos, binti wa rais wa zamani wa Angola, ambaye alitengeneza utajiri wake kwa kuwekeza katika kampuni mbalimbali za Angola wakati wa uongozi wa baba yake.
Katika orodha hii, nchi za Afrika Mashariki hazikuweza kutoa hata tajiri mmoja. Miaka ya karibuni, tajiri namba moja kutoka Tanzania, Mo Dewji, amekuwa akitajwa kwenye orodha ya matajiri wakubwa Afrika, lakini hakuwemo kwenye orodha hii.
Orodha ya matajiri hao wakubwa zaidi barani Afrika ni kama ifuatavyo kutoka wa kumi na tano mpaka wa kwanza.
15. Youssef Mansour
Net worth: $1.9 billion
Age: 75
Location: Egypt
Industry: Industrial
14. Isabel dos Santos
Net worth: $1.7 billion
Age: 47
Location: Angola
Industry: Investment
13. Yasseen Mansour
Net worth: $2.3 billion
Age: 59
Location: Egypt
Industry: Industrial
12. Koos Bekker
Net worth: $2.5 billion
Age: 67
Location: South Africa
Industry: Media
11. Patrice Motsepe
Net worth: $2.2 billion
Age: 58
Location: South Africa
Industry: Mining
10. Abdulsamad Rabiu
Net worth: $3.1 billion
Age: 60
Location: Nigeria
Industry: Manufacturing
9. Mohamed Mansour
Net worth:$3.3 billion
Age: 72
Location: Egypt
Industry: Industrial
8. Aziz Akhannouch & Family
Net worth: $3.5 billion
Age: 59
Location: Morocco
Industry: Oil & Gas
7. Naguib Sawiris
Net worth: $5.34 billion
Age: 66
Location: Egypt
Industry: Media & Telecommunications
6. Nassef Sawiris
Net worth: $5.6 billion
Age: 59
Location: Egypt
Industry: Industrial
5. Nicky Oppenheimer
Net worth: $6.53 billion
Age: 75
Location: South Africa
Industry: Diamonds
4. Johann Rupert
Net worth: $6.64 billion
Age: 70
Location: South Africa
Industry: Luxury
3. Issad Rebrab
Net worth: $7.5 billion
Age: 76
Location: Algeria
Industry: Industrial
2. Mike Adenuga
Net worth: $7.7 billion
Age: 67
Location: Nigeria
Industry: Oil and Telecommunications
1. Aliko Dangote
Net Worth: $13.5 billion
Age: 63
Location: Nigeria
Industry: Manufacturing and Industrial