Kundi la muziki wa kizazi kipya katika miondoko ya Hip Hop lenye maskami yake maeneo ya kinondoni jijini Dar es salaam limeweka wazi ujiowake mpya katika tasnia ya muziki wa hip hop.

Akizungumza na Bongo Radio, kiongozi wa kundi hilo kwa sasa (Beca Title) alieleza kwamba,baada ya kimya kingi B.O.B MICHARAZO imekuja kivingine katika fani. Alieleza kwamba kwa sasa kundi limekua na muonekano mwingine kutokana na baadhi ya wasanii kujitoa katika kundi.

Akieleza sababu ya baadhi ya wasanii kujitoa katika kundi, alisema ni kutokana na maswala ya udhamini, ambapo mdhamini aliekuwepo hapo awali kwa sasa hayupo tena, licha ya kutoweka wazi sababu ya mdhamini huyo kujitoa aliongeza kwa kusema kua ubora wa kazi za kundi bado utaendelea kuwa kama ilivyokua awali na amewataka mashabiki waendelee kuungamkono kazi za B.O.B kama kawaida. Alieleza kwa uchache baadhi ya wasanii waliojitoa ni pamoja na Mr. Blue, Nyandu Tozzy, Emba na wengineo.

Beca Tittle amekanusha kuhusu kile alichokiita uzushi uliozagaa kwamba kundi limevunjika kutokana na ugomvi wa kimaslahi kati yao. Pia alieleza kwamba kuna maneno yameenea kwamba kuna hali ya kutoelewana baina yake na Mr. Blue, ameeleza hamna ugomvi wowote kati yao na bado wapo katika mawasiliano mazuri tu.

“Sio kinyonge” ni ngoma walioiachia ikiashiria kuvunja ukimya uliodumu kwa muda mrefu,ngoma ambayo inafanya vizuri katika vituo mbalimbali vya radio na TV. Beca Title anaendelea kusisitiza kwamba B.O.B MICHARAZO bado ipo na kazi zinaendelea kama kawaida. Ameongeza kwa kusema kwamba kwa sasa nguvu itakua ya juu zaidi kuliko hapo awali, na kwakuthibitisha hilo ameeleza kwamba kuna kazi nyingi ambazo zinatarajiwa kuachiwa hivi punde,kazi ambazo zimefanyika katika studio mbalimbali wakishirikiana na wasanii mbalimbali. 

Aliweka wazi kwa kuwataja wasanii wanao unda kundi hilo kwa sasa ni Beca Tittle, Blood Gaza, Criss The Don, Uswege Master na Baby Mc. Alimalizia kwa kuwataka mashabiki wa kundi hilo waendelee kusupport harakati za B.O.B. lakini pia wakae mkao wa kula kwani kuna kazi nyingi kali zinakuja.

Previous article‘Coming 2 America’: Eddie Murphy Is Prince Akeem Again In First Look Image
Next articleThis “Naked” Microtrend Is Steadily Taking Over