Musoma. Watu 39 wamefariki dunia huku 79 wakijeruhiwa kwenye ajali iliyohusisha magari matatu eneo la Sabasaba, Wilaya ya Butiama, mkoani Mara.

Miongoni mwa waliofariki dunia yumo Mratibu wa ugonjwa wa Ukimwi wa Mkoa wa Mara, Dk Anatoria Ntangeki.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Philip Kallangi alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo jana na kwamba marehemu ni 36 na majeruhi 79.

 
News by : Staff Reporter


Copyright © 2011 — Bongo Radio