Chicago
London
Dar Es Salaam
 
 

Mfalme Wa Mipasho Mzee Yusuf Aiteka DMV Nchini Marekani Kwa Show Kabambe

News by : Staff Reporter
 
06 Feb, 2012 22:40:18
 
//
 

Mfalme wa Mipasho nchini Tanzania ambaye pia ni kiongozi wa kundi la Jahazi Modern Taarab Mzee Yusuf, ameendelea kutoa burudani ya kuvutia iliyokonga mioyo ya mamia ya wapenzi wake kutoka Washington DC, Maryland, Virginia na miji mingine ya karibu nchini Marekani.

 

Show hiyo ambayo ilihudhuriwa na umati mkubwa wa watu ilifanyika siku ya Jumamosi tarehe 4 Februari 2012 katika ukumbi wa Rendez Vous Banquet Hall katika mji wa Rockville, Maryland.

 

 

Mzee Yusuf ambaye yuko nchini Marekani kwa ziara ya utumbuizaji katika miji mbalimbali, hii ilikuwa ni onyesho lake la pili kulifanya nchini hapa baada ya onyesho kwanza kufanyika katika mji wa New York City wiki moja iliyopita.

 

Nyuso za furaha zionekanazo kutoka kwa wapenzi wake na wahudhuriaji wengine katika maonyesho yake yote mawili ambayo yameshafanyika, inaonyesha ni jinsi gani Mzee Yusuf ameweza kukonga nyoyo za wengi hata wale ambao si wapenzi wa muziki wa Taarab.

 

Picha zote kwa hisani ya VIJIMAMBO Blog.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 
 
 
 
 
Copyright © 2011 Bongo Radio. Subsidiary of Bongo Media Group. All Rights Reserved
Valid XHTML 1.0 Transitional