Chicago
London
Dar Es Salaam
 
 

Ngoma Africa Band Watoa Nyimbo Mpya Kusheherekea Miaka 50 Ya Uhuru

News by : Staff Reporter
 
06 Nov, 2011 23:41:45
 
//
 

Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya "Ngoma Africa band" aka FFU yanye maskani yake nchini Ujerumani wameachia hewani CD mpya inayojumuisha nyimbo za kusheherekea miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara.

 

Nyimbo zilizomo katika CD hiyo ni utunzi na uimbaji wake kiongozi wa bendi hiyo Kamanda Ras Makunja akiimba kwa kushirikiana na Chris-B,  ambaye ni mpiga solo wa bendi hiyo.

 

Nyimbo hizo tayari zinaweza kupatikana na kusikika katika blog mashuuri ya Michuzi. Pia inapatikana kupitia vituo vya Redio vya Deutche Welle mjini Bonn nchini Ujerumani, Radio VOA ya Washington DC nchini Marekani na  Radio Free Africa ya jijini Mwanza nchini Tanzania.

 


Nyimbo hizo ambazo zinaweza kutumika kutoa burudani kwa wananchi katika shamra shamra za miaka 50 ya uhuru wa Tanzania.

 

Nyimbo hizo mbili ambazo zinajulikana kwa jina la Miaka 50 Uhuru iliyo katika mtindo wa Rhumba na nyingine yenye jina la 50 Uhuru Shangwe iliyo katika mtindo wa Dansi.

 

Pia unaweza kuzisikia nyimbo hizo kupitia tovuti ya bendi ya Ngoma Africa inayopatikana kupitia Zinasikia www.ngoma-africa.com au http://www.ngoma-africa.com

 
 
 
 
 
Copyright © 2011 Bongo Radio. Subsidiary of Bongo Media Group. All Rights Reserved
Valid XHTML 1.0 Transitional