Shilole Muigizaji Na Mwanamuziki Aliyefanikiwa Kwa Muda Mfupi
News by : Staff Reporter
31 Jul, 2012 19:43:16
HAKUNA ubishi kuwa Shilole ambaye hivi sasa anavuma katika muziki wa mduara alianza kama muigizaji wa filamu lakini baadaye kipaji kingine kiliibuka na kuonekana bora zaidi ya kipaji cha awali.
Mwigizaji na mwanamuziki huyo Zuwena Mohamed 'Shilole', hivi sasa anapata shoo nyingi na zenye fedha nyingi ukilinganisha na wasanii wengine wa muziki wa kizazi kipya, mduara na taarabu licha ya kwamba ni mgeni katika fani hiyo.
Kwa wanaofuatilia filamu watakumbuka jinsi alivyofanya kweli katika Fair Decision akicheza na Ray, Johari na wengineo, ikifuatiwa Crazy Of Love aliyocheza na Basupa, David Mjata na wengineo, Pigo aliyocheza na Cloud na Aunty Ezekieli kabla ya kuibukia katika Bed Rest akicheza na Ray, Thea, Johari na Mainda.
Licha ya mafanikio hayo Shilole anasema baada ya kujiongezea fani nyingine na kufanya vizuri, ni kama kafungua njia kila mwigizaji wa kike anataka kuimba japo hawana uwezo huo.
Anasema kuwa wanapoona Shilole anakataa viuno wanajua kuwa kila msanii atakata viuno tu na kuwa mwanamuziki mkali.
"Najivunia kuwa na vipaji vingi lakini nawapa pole wenzangu toka nimefungua njia na kuanza kuimba naona watu wanakurupuka na kuingia katika fani ya uimbaji, sikukurupuka nilijipanga kwa ajili ya kazi na kazi inaonekana," anatamba.
"Napata shoo ambazo hata wasanii wakubwa hawapati, mimi si kama hawa wakataa viuno wanaoiga tu baada ya kumuona Shilole, sifanyi maigizo nafanya kazi inayokubalika katika jamii" anasema na kuongeza kuwa kwake filamu na muziki ni biashara.
Shilole pia amekamilisha nyimbo nyingine alizoimba kwa kuwashirikisha wasanii Mzee Yusuf (Kachumbari), Barnaba (Surprise), Q Chilla (Dudu) na Richi Mavoko na Kitokololo (Viuno).
Akizungumzia maisha yake halisi nyota huyo aliweka wazi kuwa ndoa yake na mfanyabiashara wa mafuta wa mkoani Tanga, itafungwa mapema mwezi huu wa Julai, kutokana na mchakato unaoendelea kufanyika.
Akizungumzia ishu hiyo Shilole, alisema kuwa ameamua kuweka wazi ndoa yake kwani anapenda mashabiki wake waweze kujua nini kinachoendelea katika maisha yake.
ìNilikuwa sitaki watu waweze kujua kuhusu ndoa yangu, kwa sababu siyo tangazo lakini nimeona bora niweke wazi ili mashabiki wangu waweze kujua ishu hiyo ambayo itakuwa ya kihistoria sanaî alisema.
Hata hivyo msanii huyo hakutaka kumtaja jina mume wake mtarajiwa kwa kile alichodai kuwa ni mapema na anataka iwe zawadi kwa mashabiki wake.
Yanayomhusu Msanii huyo mwenye watoto wawili Rahma na Joyce, ndoa yake ya kwanza alifunga mwaka 2005 kabla ya kutalikiana miaka mitatu baadaye, alizaliwa huko Igunga, Tabora mwaka 1986.
Elimu yake ya msingi na Sekondari aliipata Igunga kabla ya kuja Jijini Dar es Salaan na kujiunga na Chuo kimoja cha masuala ya hoteli na utalii kilichopo Magomeni alipopata cheti ambapo mbali na filamu anafanya kazi ya uhudumu katika hoteli ya Peakock iliyopo katikati ya Jiji la Dar es Salaam.
Akiwa anavutiwa na muigizaji wa Kinigeria Ini Edo, Zuwena ni mtoto wa mwisho kati ya familia ya watoto watano, huku wazazi wake Mohamed Yussuf na mama Pili Yussuf walifariki kwa ajali ya gari ya abiria, walipokuwa wakisafiri kutoka Igunga kwenda Tabora mwaka 1996.
Mduara Video: Shilole Feat. Q Chillah - Lawama
SOURCE: Mwananchi
Warning: include(/home/bongorad/public_html/includes/comment_box.php) [function.include]: failed to open stream: Permission denied in /home/bongorad/public_html/news_details.php on line 195
Warning: include(/home/bongorad/public_html/includes/comment_box.php) [function.include]: failed to open stream: Permission denied in /home/bongorad/public_html/news_details.php on line 195
Warning: include() [function.include]: Failed opening 'includes/comment_box.php' for inclusion (include_path='.:/usr/lib/php:/usr/local/lib/php') in /home/bongorad/public_html/news_details.php on line 195