Chicago
London
Dar Es Salaam
 
 

Tanzania Yaonywa Na Marekani Kuacha Kusajili Meli Za Mafuta Za Iran

News by : Staff Reporter
 
30 Jun, 2012 00:25:02
 
 

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeonywa kuacha mara moja kuzisajili meli za mafuta za nchi ya Iran ambayo imewekewa vikwazo vya kiuchumi na jumuiya ya kimataifa ikiongozwa na Marekani na nchi za Ulaya.

 

Onyo hilo limetolewa na Mwakilishi Howard Berman kutoka jimbo la California anayewakilisha chama cha Democrats anachotoka Rais Barack Obama katika Bunge la Marekani ambaye pia ni mjumbe wa juu wa Kamati ya Mambo ya Nje katika Baraza la Wawakilishi la Marekani.

 

 

Katika barua yake aliyomtumia Rais Jakaya Kikwete, Mwakilishi huyo amesema Tanzania iko katika hatari ya kuwekewa vikwazo na nchi ya Marekani pamoja na kuathiri uhusiano mzuri baina ya nchi hizi mbili iwapo Tanzania haitoacha kuzisajili meli kubwa za kubebea mafuta za Marekani.

 

Ameendelea kusema kitendo hicho kinachofanywa na Serikali ya Tanzania kina nia ya kuisaidia nchi ya Iran iweze kuepuka vikwazo iliyowekewa na nchi za Kimataifa ili iendelee na mpango wake wa kutengeneza silaha za nyuklia ambazo zitasaidia kuendeleza ugaidi duniani.

 

Pamoja na kuwekewa vikwazo vya kiuchumi, Mwakilishi huyo amesema pia Tanzania inaweza kunyimwa misaada yote kiuchumi kutoka kwa Marekani na nchi nyingine marafiki.

 

Onyo hilo kutoka kwa Mwakilishi huyo limetokana na taarifa mbalimbali zinazoonyesha kuwa meli karibia kumi kutoka kampuni ya meli za mafuta ya Iran au National Iranian Tanker Company zimesajiliwa hivi karibuni katika Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania.

 

Usajili huo utazifanya meli hizo zikwepe vikwazo hivyo vya kiuchumi kiurahisi zaidi kutokana na kubeba bendera ya Tanzania.


Warning: include(/home/bongorad/public_html/includes/comment_box.php) [function.include]: failed to open stream: Permission denied in /home/bongorad/public_html/news_details.php on line 195

Warning: include(/home/bongorad/public_html/includes/comment_box.php) [function.include]: failed to open stream: Permission denied in /home/bongorad/public_html/news_details.php on line 195

Warning: include() [function.include]: Failed opening 'includes/comment_box.php' for inclusion (include_path='.:/usr/lib/php:/usr/local/lib/php') in /home/bongorad/public_html/news_details.php on line 195
 
 
Copyright © 2011 Bongo Radio. Subsidiary of Bongo Media Group. All Rights Reserved
Valid XHTML 1.0 Transitional