Mkenya Amuua Rafiki Yake Na Kumla Moyo Na Ubongo Wake Nchini Marekani
News by : Staff Reporter
31 May, 2012 15:12:14

Mwanafunzi kutoka nchini Kenya anayesoma chuo cha Morgan State University katika jimbo la Maryland nchini Marekani aitwaye Alexander Kinyua amemuua na kisha kula ubongo na moyo wa marehemu huyo anayeitwa Kujoe Agyei-Kodie aliyekuwa anaishi naye nyumba moja.
Mauaji hayo ambayo yamewashtua watu wengi katika jimbo hilo la Maryland na Marekani nzima, yametokea huku kukiwa kuna matukio mengine kama hilo ambayo yametokea katika jimbo la Florida pia nchini Marekani na nchi ya jirani ya Canada wiki hii.
Alexander Kinyua ambaye kwa hivi sasa anashikiliwa na wana usalama amekiri kwa wapepelezi wa Polisi kuhusika na mauaji hayo ya kutisha.
Mwanafunzi huyo mwenye miaka 21 ambaye alifikishwa mahakamani siku ya Jumatano ya tarehe 30 Juni 2012 huku akikabiliwa na shitaka hilo la mauaji ambalo adhabu yake ya juu ni kifungo cha maisha au kifo.
Kukamatwa kwa muuaji huyo kulitokana na kaka wa mtuhumiwa huyo kukuta mabaki ya mwili wa binadamu ambayo ni mikono na kichwa nyumbani kwao na hivyo kumtaarifu baba yao ambaye alipiga simu Polisi kulikofanikisha kukamatwa kwa Alexander.
Mpaka sasa haijulikana sababu kuu za mauaji hayo ya kinyama au kitu gani kilichosababisha mtuhumiwa kufikia kumuua rafiki yake huyo.
Warning: include(/home/bongorad/public_html/includes/comment_box.php) [
function.include]: failed to open stream: Permission denied in
/home/bongorad/public_html/news_details.php on line
195
Warning: include(/home/bongorad/public_html/includes/comment_box.php) [
function.include]: failed to open stream: Permission denied in
/home/bongorad/public_html/news_details.php on line
195
Warning: include() [
function.include]: Failed opening 'includes/comment_box.php' for inclusion (include_path='.:/usr/lib/php:/usr/local/lib/php') in
/home/bongorad/public_html/news_details.php on line
195