Tupac Shakur Afufuliwa Stejini Kwa Kutumia Teknolojia Ya Hologram
News by : Staff Reporter
17 Apr, 2012 17:59:38
Msanii wa Hip-Hop ambaye mpaka hivi sasa anasemakana ndie rapa bora na anayependwa na wengi aliyepata kutokea katika ulimwengu wa muziki wa rap na hip-hop Hayati Tupac Shakur alifufuliwa na kushiriki kwenye tamasha la Coachella Valley Music & Arts katika jimbo la California nchini Marekani.
Teknolojia hiyo ya hologram ambayo iliweza kuleta taswira halisi ya Tupac Shakur kwenye 3D huku akishiriki katika uimbaji wa nyimbo zake zilizowahi kutamba sana duniani kama "Haily Mary" na "Gangsta Party" huku akiamsha mshangao mkubwa, hisia na furaha kutoka kwa wahudhuriaji wote wa tamasha hilo kubwa la muziki.
Taswira hiyo ya Tupac Shakur iliingia stejini kujiunga na wasanii wenzake maarufu duniani aliokuwa nao Death Row Records, Snoop Dogg na Dr. Dre na kushiriki pamoja katika kutoa burudani kwa wahudhuriaji.
Kuna tetesi kuwa taswira hiyo ya hayati Tupac Shakur inayotumia teknolojia ya hali ya juu na kisasa ya hologram itashiriki kwenye ziara za wasanii hao wawili wakubwa wa Hip-Hop ambao ni Snoop Dogg na Dr. Dre katika miji mingine mbalimbali duniani.
Warning: include(/home/bongorad/public_html/includes/comment_box.php) [function.include]: failed to open stream: Permission denied in /home/bongorad/public_html/news_details.php on line 195
Warning: include(/home/bongorad/public_html/includes/comment_box.php) [function.include]: failed to open stream: Permission denied in /home/bongorad/public_html/news_details.php on line 195
Warning: include() [function.include]: Failed opening 'includes/comment_box.php' for inclusion (include_path='.:/usr/lib/php:/usr/local/lib/php') in /home/bongorad/public_html/news_details.php on line 195